Mazingira yahitaji hatua haraka

Jopo la Umoja wa Mataifa la wataalamu wa sayansi ya hali ya hewa, limeonya leo kuwa mabadiliko makubwa yanatokea katika hali ya hewa duniani na haitawezekana kurejesha hali ya zamani iwapo gesi zinazozidisha joto duniani, hazitaondoshwa kabisa ufikapo mwisho wa karne.
Ripoti iliyokubaliwa kwenye mkutano mjini Copenhagen, imechapishwa leo.
Dakta Peter Gleick ni mwana-sayansi wa mabadiliko ya hali ya hewa ambaye ameiona ripoti hiyo.
Aliiambia BBC, ushahidi wa kisayansi ni mzito sasa, kuwa binaadamu ndiye chanzo cha mabadiliko ya hali ya hewa:
"Bila ya shaka watu wasioamini kuwa wanaadamu ndio wanasababisha mabadiliko ya hali ya hewa, hawataki kusikiliza sayansi.
Kuna maswala magumu ya kisiasa yanahitaji kuamuliwa, lakini siyo ya kisayansi tena.
Ushahidi katika sayansi ni thabiti - kwamba hali ya hewa inabadilika; kwamba wanaadamu ndio wanayosababisha hayo.
Na kwamba ikiwa hatuchukui hatua sasa, basi totaona matokeo makubwa na hasara itakuwa kubwa kwa watu na dunia yenyewe."
Na Waziri wa Mashauri ya nchi za Nje wa Marekani, John Kerry, alisema wale wanaodharau sayansi kuhusu hali ya hewa iliomo kwenye ripoti hiyo, wanahatarisha maisha yetu, watoto na wajukuu wetu.
Madaktari wa Kenya walalamikia utayari wa kupambana na homa ya Ebola
Madaktari wa Kenya wamelalamikia utayari wa serikali kupambana na ugonjwa wa Ebola wakati tayari ugonjwa huo umesababisha vifo vya watu elfu 3 katika nchi za Afrika Magharibi. Chama cha maofisa wa maabara wa Kenya kimesema mjini Mombasa kuwa Kenya ina hatari ya kukumbwa na ugonjwa huo kutokana na kutojiandaa vizuri.
Kwingineko ugonjwa wa Ebola unaendelea kuleta changamoto. Nchini Liberia ofisa wa pili wa tume ya kulinda amani ya Umoja wa Mataifa amethibitishwa kuambukizwa Ebola na sasa maofisa wote wenye hatari wamewekwa kwenye karantini, ili kuhakikisha ugonjwa huo hauenei zaidi. Marekani nayo imetangaza kuwa itaanza ukaguzi mkali katika viwanja vya ndege vitano vinavyopokea abiria kwa wingi kutoka kwenye nchi zilizoathiriwa zaidi na maambukizi, baada ya mgonjwa wa kwanza kutoka Liberia aliyekuwa anatibiwa katika hospitali moja ya Texas kufariki dunia.
Benki ya dunia imetoa ripoti kuwa, ugonjwa wa Ebola unaziletea hasara kubwa kwa nchi tatu za Afrika magharibi. Hadi kufikia mwishoni wa mwaka huu, athari ya ugonjwa huo kwa uchumi inawezekana kufikia dola za marekani bilioni 32.6.

No comments:
Post a Comment